HIV ni nini?


HIV ni jina la virusi na ni ugonjwa unaosababishwa

H = binadamu – watu wanaopata
I = Upungufu wa kinga-Unashambulia kinga yako ya mwili
V = Virusi-Vinavyokufanya uugue


Namna gani ninapata HIV?


Huwezi kutambua kwa kuangalia tu kama mtu ana HIV. Watu wenye virusi vya ukimwi wanajisikia wenye afya na wazima

HIV inaishi katika damu, majimaji kwenye viungo vya uzazi na katika maziwa ya mama. Unapata HIV kama mojawapo ya vifuatavyo vikiingia katika mfumo wako wa damu. Njia kuu za kupata HIV ni kutoka:
● Kutotumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi
● Kuchangia sindano, sirinji ama vijiko kujidunga madawa ya kulevya.
● Kujichora tattoo kwa vifaa visivyo salama, kujitoboa mwili ama sherehe ya kinda into mwingine ambapo watu hudungwa kwenye ngozi.
● Maziwa ya mama
● Mwingiliano wa damu ya watu wawili tofauti kama vile kuongezewa damu ama kuwekewa kiungo katika nchi ambazo hazipimi HIV. Kuongezewa damu na kuwekewa kiungo nchini Australia kuko salama kama taratibu zote zikifuatwa.

Huwezi kupata HIV kwa:
● Kukumbatiana
● Kukohoa ama kupiga chafya
● Kuchangia chakula ama kinywaji
● Kula chakula kilichopikwa na mtu mwenye HIV
● Kuchangia damu au taratibu za hospitalini nchini Australia
● Kuchangia choo ama bafu na mtu mwenye HIV
● Kuumwa na mnyama ama mdudu
● Kukutana na watu wenye HIV
● Mabwawa ya kuogelea ama gym

Je, HIV inafanya nini kwa mwili wangu?


HIV inashambulia kinga yako ya mwili. Kinga yako ya mwili inapambana na maambukizi na kuulinda mwili wako usiugue. HIV inadhoofisha mfumo wako wa kinga na unashindwa kukulinda. Kama hauna dawa za HIV, unaweza kuugua sana.

Je, HIV na AIDS ni kitu kimoja?


Hapana
HIV ni virusi seli za kinga ya mwili
AIDS siyo virus

AIDS ni ugonjwa nadra unaoshambulia mwil wakati kinga yako ya mwili ikiwa dhaifu. Hii inatokea tu wakati virusi vya HIV vinapoua sehemu kubwa ya seli za kinga. Hii inaweza kutokea baada ya miaka mingi.

AIDS ni nadra sana nchini Australia kwa sababu dawa zinaweza kuizuia.

Kuwa na virusi vya HIV haimanishi utakufa kwa AIDS nchini Australia.

Ninatambuaje kama nina HIV?


Namna pekee ya kutambua kama una HIV ni kupima damu.
Kama vipimo vinaonyesha ‘negative,’ hauna HIV
Kama vipimo vikionyesha ‘positive,’ una HIV

Watu wengi hawajui kama wana HIV kwa sababu wanajisikia vizuri. Lakini unapopata HIV unaweza kuwa na:

● kichwa kugonga
● homa
● uchovu
● kuvimba kwa tezi
● kuwashwa koo
● vipere (ukurutu) katika ngozi
● maumivu ya misuli na maungo
● Madonda mdomoni
● Madonda sehemu za siri
● Kutokwa na jasho usiku
● kuharisha

Lakini dalili hizi zinaweza kusababishwa na mafua, baridi kali ama ugonjwa mwingine wowote. Kama unafikiri unaweza kuwa na HIV ni muhimu umwone daktari na uombe vipimo.

Nafanyaje kama mimi ni HIV positive?


Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuongea na daktari. Wanaweza pia kuamua kama unahitaji kuongea na mtu mwingine kama vile mshauri nasaha kama utapenda.

Daktari atakupatia dawa za HIV. Dawa hizi zitakuwezesha kuishi muda mrefu, maisha yenye afya.

Je, HIV inaweza kutibika?


HIV haiwezi kutibika ila madawa yanaweza kuitibu.

Dawa zinapunguza kiasi cha virusi vilivyoko kwenye damu hadi kiasi cha chini, haviwezi kuonekana hata kwa kutumia darubini. Tunaiita hii ‘undetectable viral load”(kiasi cha virusi visiyoonekana) na hii ina maana kwamba hutaweza kuugua virusi na ukabakia kuwa urefu wa maisha ya kawaida. Kama ukiendelea kutumia dawa sawasawa, hii ina maana kwamba hautaweza kumwambukiza mtu mwingine.

Nawezaje kujilinda kutoambukizwa HIV?


● Pima na chunguza kama wewe ama mpenzi wako ana HIV: Kama una mpenzi Zaidi ya mmoja (ama mpenzi wako ana mahusiano ya kimapenzi na watu wengine, chukua vipimo mara kwa mara. Uwezekano wa kuambukizwa HIV ni mkubwa sana kulingana na idadi ya wapenzi unaokuwanao
● Tumia kondomu
● Pima na pata matibabu ya magonjwa mengine ya maambukizi ya kingono. Kuwa na maambukizi ya kingono inaongeza uwezekano wa kupata HIV ama kumpatia mtu mwingine. Mwombie mpenzi wako apime na kutibiwa maambukizi mengine ya kingono.

● Muulize daktari wako kuhusu pre-exposure prophylaxis (PrEP). PrEP ni dawa inayokukinga kupata HIV. Ni kwa ajili ya watu ambao hawana HIV lakini wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

Hatari kubwa maana yake:
o Mtu mwenye mpenzi mwenye HIV
o Watu ambao wana wapenzi zaidi ya mmoja
o Mwanaume anayeshiriki mapenzi na mwanaume mwenzake.
o Watu ambao hawatumii kondomu mara kwa mara
o Watu wanaochangia sindano, sirinji, maji na vijiko vya kujidungia madawa ya kulevya.

● Tumia tu vifaa salama vya kujidungia madawa na maji: Usichangie vifaa hivyo na wengine. HIV inaweza kusambazwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine hata katika matone ya damu madogo kuonekana katika sindano ya kuchomea
● Kujichora michoro na kutoboa mwili: Tumia tu studio zenye leseni ambapo sindano na vifaa vinginevyo vinasafishwa sawasawa ama kutupwa baada ya matumizi. Hakikisha kila mara wanatumia wino mpya kwako

● Kuongezewa damu na taratibu zingine za kitabibu: Nchini Australia damu yote, mazao ya damu na viungo vinapimwa na viko salama. Ila kuongezewa damu, mazao ya damu na viungo vinaweza visiwe salama katika nchi nyingine.

Nawezaje kuhakikisha kwamba simwambukizi mtu mwingine HIV?


● Ongea na daktari wako kuhusu kutumia dawa za HIV: Dawa za HIV zinasaidia kupunguza kiasi cha virusi vya HIV vilivyoko katika damu. Kiasi cha virusi vya HIV kinapokuwa kidogo, huwezi kumpatia mtu mwingine virusi vya ukimwi. Hii inatambulika kama Matibabu kwa Njia ya Kinga (TasP)
● Pima kila mara: hata kama unatumia madawa ya HIV, unapaswa kuwa unapima kila mara. Kuna aina tofauti za virusi vya HIV na inawezekana kuwa na aina zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Dawa zinaweza kutakiwa kubadirishwa kama hii ikitokea.
● Pima magonjwa mengine ya maambukizi ya kingono: dawa za HIV hazikuzuii kupata magonjwa mengine ya maambukizi ya kingono. Pima mara kwa mara maambukizi mengine ya kingono na pata matibabu kama vipimo vikionyesha kwamba umeambukizwa. Mpenzi wako anapaswa kupimwa na kupewa matibabu pia.
● Tumia kondomu: Tumia kondomu kila mara unapofanya mapenzi
● Usichangie sindano, sirinji, vijiko vya kujidungia madawa ya kulevya
● Kunyonyesha: Kama unatumia madawa ya HIV na unataka kumnyonyesha mtoto wako, ongea na daktari wako wa HIV

Je, ninawajibika kumwambia mtu yeyote kama nina HIV?


Kwa sheria ni lazima umjulishe:
● Mpenzi ama wapenzi wako. Katika baadhi ya majimbo nchini Australia, ni lazima umweleze mpenzi wako kabla ya kufanya mapenzi nao. Kila jimbo ni tofauti hivyo ni vizuri ulichunguze kabla hujaenda huko
● Jeshi la Ulinzi la Australia. Hauwezi kujiunga kama una HIV
● Kama wewe ni rubani
● Kama ukinunua baadhi ya bima kama vile bima ya afya ama kusafiria.
● Kama unataka kuchangia damu ama kiungo kama vile figo. Huwezi kuchangia damu ama kiungo kama una HIV
Haulazimiki kumweleza:
● Mkuu wako
● Wafanyakazi wenzako
● Mwenzako mnayeishi chumba kimoja
● Familia
● Mwenye nyumba
● Mwalimu
● Mwanadarasa mwenzako
● Rafiki zako

Watu unaoweza kuwambia ni:
● Daktari wako ili akusaidie kupima na matibabu
● Mshauri nasaha ama watu wengine ambao ni sehemu ya huduma kwa wagonjwa wa HIV ili wakusaidie

Wapi naweza kupata msada na ushauri?


Kuna makundi mengi ya HIV Australia yanayoweza kukupa ushauri na msaada.


Get support from the HIV community

More information