Hepatitis B ni nini?

Hepatitis B ni jina la kirusi na jina la ugonjwa utokanao na kirusi hicho.

Hepatitis B inalifanya ini lako kuugua. Kunywa pombe kupita kiasi kunasababisha ugonjwa huu; ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya, kemikali na virusi vinginevyo.

Ini lako ni muhimu sana kwa afya yako. Linapoharibika, haliwezi kufanya kazi ipasavyo na linaweza kukufanya uugue sana

Hepatitis B wakati mwingine hujulikana kama “hep B”


Ninapataje Hepatitis B?


Hepatitis B inaambukizwa wakati damu ama majimaji ya via vya uzazi kutoka kwa mtu mwenye hepatitis B vinapoingia katika mfumo wako wa damu.Unaweza kupata hepatitis B hata kama kiasi cha damu ama majimaji vya via vya uzazi ni kidogo sana kuonekana.

Kwa vichanga na watoto wadogo

● mama mwenye hepatitis B anaweza kumwambukiza mtoto anapozaliwa kama asipopewa chanjo mapema.
● Mtoto mwenye hepatitis B anaweza kumwambukiza mtoto mwingine ambaye hajapewa chanjo, kupitia majeraha ambayo hayajafunikwa na madonda.

Kwa watu wazima

Unaweza kupata hepatitis B kutoka

● Ukeni, njia ya haja kubwa unapofanya ngono bila kondomu ama ngono kwa mdomo
● Kuchangia sindano, sirinji ama vifaa vingine vya kijidunga kama vijiko
● Kujichanja michoro ama kujitoboa mwilini kwa vifaa visivyo salama
● Kuchangia miswaki, nyembe au vifaa vya kucha
● Ajali kwa kujichoma na sindano ama kurukiwa na damu yenye maambukizi
Huwezi kupata hepatitis B kutokana na:

● Kukumbatiana
● Kubusiana
● Kuchangia chakula na vyombo vya kupikia
● Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye hepatitis B
● Kung’atwa na wanyama ama wadudu
● Jasho
● Kufua nguo
● Kupiga chafya ama kukohoa
● Kuchangia mabafu au vyoo
● Mabwawa ya kuogelea

Ninatambuaje kama nina hepatitis B?


Watu walio wengi hawana ishara ama dalili na wala hawajisikii kuugua. Njia pekee ya kutambua ni kuchukua vipimo.

Unapopata hepatitis B kwa mara ya kwanza unaweza:

● Kutapika

● Kuwa na homa

● Kukosa hamu ya chakula

● Kuwa na mkojo mweusi

● Maumivu ya ini (chini ya mbavu upande wa kulia)

● Maumivu kwenye maungio

● Macho na ngozi ya njano

Hepatitis B inafanya nini kwenye mwili wangu?


Hepatitis inaingia kwenye seli katika ini lako na kulifanya liugue. Mwili unafanya kazi sana kupambana na virusi ndani ya ini. Mapambano haya yanaharibu ini na, kwa miaka mingi, yanaweza kufanya ini kusimama kufanya kazi.
Kwa watu wazima wengi, mwili unaondoa hepatitis B ndani ya miezi sita baada ya kuambukizwa, na huwezi kuipata tena.

Ila kwa watoto wadogo na wakati mwingine watu wazima, wakati mwingine mwili unashindwa kukabiriana, na hepatitis inabakia mwilini maisha yote. Hii inajulikana kama “hepatitis B iliyopea na inaweza kuharibu ini, makovu katika ini (cirrhosis) na kansa ya ini. Dawa zinaweza kupunguza madhara na kuzuia kansa ya ini.

Ninafanyaje nikiwa na hepatitis B?


Ni lazima umwone daktari wako kila miezi sita hadi kumi na mbili, hata kama unajisikia vizuri. Hii ni kwa sababu hepatitis B haikufanyi kuwa mgonjwa. Unapojisikia mgonjwa ni kwa sababu tayari ini limeshaharibika.

Pamoja na vipimo vya damu, daktari wako anaweza kufanya Fibroscan.* Fibroscan* ni kipimo cha picha ya ini kinachomwonyesha daktari wako kuna madhara katika ini yako ama makovu katika ini (cirrhosis) na limeharibika kiasi gani. Kisha daktari wako ataamua kama unahitaji dawa ama unahitaji kwenda kwenye kliniki ya ini ama kuonana na daktari maalum wa ini.

Je, hepatitis B inaweza kutibiwa au kupona?


Ndiyo, hepatitis B inaweza kutibiwa.

Ila siyo watu wote wenye hepatitis B wanahitaji dawa. Daktari wako atakwambia kama unahitaji dawa.

Dawa haziwezi kutibu hepatitis B. Ila inaweza kudhibiti uharibifu wa ini, kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya ini na kulisaidia ini kujitibu.

Ongea na daktari wako kuhusu ni dawa ipi itakufaa zaidi.

Nawezaje kulisaidia ini langu?


  • Kunya pombe kidogo au kutokunywa kabisa
  • Kula mlo kamili wenye afya, na isiyo na mafuta mengi.
  • Acha ama punguza matumizi ya sigara.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara
  • Dhibiti msongo wa mawazo na omba msaada
  • Mweleze daktari wako kama unatumia dawa zozote kama vile miti shamba, vitamin, ama madawa ya kichina. Baadhi ya dawa hizi zinaweza kudhuru ini, hasa kama zinatumiwa kwa dozi kubwa ama kwa muda mrefu.
  • Jilinde na maambukizi mengine kwa sababu yanaweza kuathiri vibaya sana afya yako na kusababisha madhara zaidi ya ini.
  • Pata chanjo kwa ajili ya hepatitis A
  • Usichangie sindano ama vijiko vya kujidunga madawa ya kulevya
  • Tumia kondomu.

Nawezaje kuepuka kupata hepatitis B au kumwambukiza mtu mwingine?


Chanjo
Chanjo ndiyo njia sahihi zaidi ya kudhibiti hepatitis B kusambaa.

Ni salama zaidi na inakulinda zaidi ya 95% ya muda

Unapata sindano 2 au 3 kwa zaidi ya miezi 6, kulingana na umri wako.

Nchini Australia, watoto wote chini ya mwaka mmoja hupata chanjo 4 za bure kwa zaidi ya miezi 6
Chanjo inahimizwa zaidi kwa watoto wenye umri kwa kati ya 10 na 13 ambao hawakupata sindano utotoni.

Kama mama ana hepatitis B, mtoto atapewa sindano ya ziada ndani ya masaa kumi na mbili ya kuzaliwa. Hii inampatia mtoto usalama zaidi. Watoto wanapokuwa na miezi 9, wanahitaji kupimwa kuhakikisha wamekingwa na hepatitis B

Kuepuka kumpa hepatitis B mtu mwingine

● Hakikisha watu ulio na mawasiliano ya karibu wamechanjwa
● Tumia kondomu
● Usichangie miswaki, nyembe ama vitu vingine binafsi ambavyo vinaweza kuwa na damu, ikiwa ni pamoja na damu kavu.
● Usiruhusu watuwengine kugusa majeraha yako ya wazi mpaka wawe na glovu.
● Usichangie sindano, sirinji ama vifaa vinginevyo vya kujidungia madawa ya kulevya.
● Usitoe damu, mbegu za kiume, viungo ama nyama za mwili
● Ongea na daktari wako kuhusu chanjo mtoto wako atahitaji kama u mzamzito au kama unahitaji kuwa na mtoto

Je, ninahitaji kumjulisha yeyote kama nina hepatitis B?


● Unatakiwa kuijulisha familia yako, watu unaoishi nao na mpenzi wako (wapenzi wako) ili waweze kupimwa na kupewa chanjo. Daktari wako anaweza kukusaidia kufanikisha hili.
● Kama unahitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Australia, ni sharti uwajulishe.
● Ni lazima uwajulishe kampuni yako ya bima. Usipowajulisha, wanaweza wasikulipe kama ukiugua ama kupata majeraha.
● Kama wewe ni mfanya kazi wa huduma ya afya anayefanya taratibu za kitabibu ambapo huwezi kuona mikono yako (kama vile daktari wa upasuaji ama wa meno) ni lazima umjulishe mwajiri wako ama msimamizi wako na kupata ushauri wa daktari bingwa.

Hulazimiki kumjulisha mkuu wako, watu unaofanya kazi nao au marafiki.

Kuwajulisha watu kama mtaalam wako wa meno au daktari wako itawasaidia kukupatia huduma sahihi, ila hili ni chaguo lako. Kama ukiamua kuwapatia, hawawezi kumweleza mtu mwingine.
Unaweza kuhitaji kuongea na watu wengine wanaoweza kukuelewa na kukusaidia. Chukua muda kuamua ni nani unaweza kumwamini.

Wapi naweza kupata msaada ama ushauri?


Kuna makundi mbalimbali ya hepatitis B nchini Australia ambao wanaweza kukupa ushauri na msaada.


Get support from the hepatitis community

More information