Kisonono ni nini?

Kisonono ni maambukizi ya kingono (STI) yanayosababishwa na bakteria ajulikanaye kama Neisseria gonorrhoea


Ninapataje Kisonono?


Unaweza kupata kisonono kwa kufanya mapenzi kupitia uke, kinyume na maumbile kwa ngono kwa mdomo na mtu mwenye kisonono.

Unaweza kupata kisonono kutoka kwa mtu mwingine hata kama hawana dalili zozote.

Mwanamke mjamzito anaweza kumwambukiza mtoto wake wakati wa kujifungua. Mtoto anaweza kupata maambukizi ya macho na anaweza kuwa kipofu.

Huwezi kupata kisonono kutoka vyoo vya umma, mabwawa ya kuogelea ya umma ama kuchangamana na watu wengine.

Kisonono inafanya nini kwa mwili wangu?


Kisonono inaweza kuambukiza koo, njia ya haja kubwa, njia ya mkojo, shingo ya kizazi na macho.

Kama isipotibiwa, kisonono inaweza kusababisha maambukizi ya ngozi na vifundo. kisonono inaweza pia kusababisha uti wa mgongo. Uti wa mgongo ni maambukizi yanayozingira ubongo
Kwa wanawake, kisonono inaweza kusababisha maambukizi hatari na kumsababishia mtoto ugumba.
Mwanamke mjamzito anaweza kukiambukiza kichanga wakati wa kujifungua. Kichanga kinaweza kupata maambukizi hatari ya machocho na kinaweza kupata upofu.

Ninatambuaje kama nina Kisonono?


Watu wengi hajui kama wana kisonono kwa sababu hawana ishara wala dalili.
Namna pekee ya kuweza kutambua una kisonono ni kupima. Kipimo chenyewe ni kipimo rahisi cha mkojo.
Namna nyingine ni ya kuchukua vipimo kutoka eneo lililoambukizwa na kuona kama lina maambukizi ya kisonono.

Ishara na dalili za kisonono

Kwa wanaume
• Kusikia kama kuwaka moto wakati wa kukojoa
• Kutokwa na uchafu katika njia ya mkojo. Uchafu huu unakuwa mara nyingi mweupe ama wa njano
• Kuvimba na kusikia maumivu katika korodani
• Wekundu katika tundu la uume
• Kutokwa uchafu kutoka njia ya haja kubwa au kusikia maumivu.
• Maambukizi ya macho.

Kwa wanawake
• Kutokwa na uchafu usio wa kawaida katika uke
• Kuvuja damu ukeni
• Maumivu wakati wa kukojoa
• Maumivu kwenye mifupa hasa wakati wa kufanya mapenzi
• Kutokwa uchafu kutoka njia ya haja kubwa na hata maumivu
• Maambukizi ya macho

Ninafanyaje kama nina Kisonono?


• Daktari wako atakupatia dawa
• Mwambie mpenzi au wapenzi wako kupima. Kama wana kisonono, wanaweza kukupatia kisonono tena ama kumpatia mtu mwingine.
• Daktari wako anaweza kukusaidia kuamua ni nani wa kumwambia kwamba una kisonono. Daktari wako anaweza kukusaidia kuwambia.
• Usifanye mapenzi na mtu yeyote, hata kwa kutumia kondomu, mpaka matibabu yako ya kisonono yatakapokamilika.

Je, kisonono inaweza kutibika ama kupona?


Gonorrhoea inaweza kutibika na kupona kwa sindano moja ya antibiotiki.
Kila mara mwambie daktari wako kama ulikuwa nje ya nchi. Hii ni kwa sababu baadhi ya aina za kisonono ni nadra sana nchini Australia na zinahitaji dawa maalum.
Unaweza kupata kisonono tena hata kama ilipona siku za nyuma.

Je, ninaweza kujilindaje nisipate Kisonono?


• Hakikisha wewe na wapenzi wako mnapimwa kisonono. Pima mara kwa mara kama una mpenzi Zaidi ya mmoja au mpenzi wako ana mahusiano ya kimapenzi na watu wengine. Kadiri ya wingi wa wapenzi , ndivyo hatari ya kupata kisonono inavyoongezeka.
• Hakikisha wewe na mpenzi wako mnatibiwa kisonono ili msiendelee kuambukizana ama kuwaambukiza watu wengine.

• Tumia kondomu wakati wa mapenzi kwa uke, kinyume na maumbile ama kwa ngono kwa mdomo. Tumia kondomu hata kwa mpenzi wako wa mda mrefu kama unafanya mapenzi na watu wengine.
• Ongea na wapenzi wapya kuhusu kutumia kondomu kabla hujafanya nao mapenzi.

Je, ninaweza kufanyaje nisimwambukize mtu mwingine Kisonono?


• Usifanye mapenzi na mtu yeyote, hata kwa kutumia kondomu, mpaka utakamilishe matibabu na hauna dalili zozote.
• Tumia kondomu kila mara unapofanya mapenzi na mpenzi mpya
• Hakikisha unachukua vipimo vya kisonono mara kwa mara kama una mpenzi zaidi ya mmoja au mpenzi wako anafanya mapenzi na watu wengine.

Ninaweza kupata wapi msaada na ushauri?


Unaweza kupata msaada kutoka:
• Kwa daktari
• Kliniki ya afya ya uzazi
• Huduma ya afya ya kijamii
• Vituo vya uzazi wa mpango

More information