Hepatitis C ni nini?

Hapatitis C ni kirus kinachoifanya ini lako liugue. Kunywa pombe kupita kiasi, kutumia madawa ya kulevya, kemiikali na virus vinginevyo vinaweza kusababisha ini lako liugue.

Ini lako ni muhimu sana kwa afya yako. Ini linapoumia ama linapoharibika linaweza lisifanye kazi vizuri na linaweza kukufanya uugue sana.

Hepatitis C wakati mwingine inajulikana kama “hep C”


Ninawezaje kupata hepatitis C?


Unaweza kupata hepatitis C kama damu ya mtu mwenye hepatitis C ikiiingia kwenye mishipa yako ya damu. Hata kama matone ya damu ni madogo sana kuweza kuonekana, unaweza kupata hepatitis C
Shughuli zenye hatari kubwa
● Kuchangia sindano, sirinji na vijiko vya chai,kujidunga madawa ya kulevya ndio njia kuu ya watu kupata hepatitis C
● Kujichora tattoo kwa vifaa visivyo salama, kujitoboa mwili ama sherehe ya kinda into mwingine ambapo watu hudungwa kwenye ngozi
● Njia ambazo mwili unatobolewa na vifaa vya matibabu visivyo salama, sindano za meno
Shuguli zenye hatari kidogo
● Mama mwenye hepatitis C anaweza kumwambukiza mototo wake wakati wa ujauzito ama wakati wa kujifungua.

● Kuchangia miswaki na nyembe
● Kujichoma sindano kwa bahati mbaya kwa wafanyakazi wa afya
Huwezi kupata hepatitis C kutoka:
● Kuchangia vyoo au mabafu
● Jasho ama kufua nguo za mtu mwenye hepatitis C
● Kuchangia visu na uma, sahani ama vikombe na glasi
● Kula chakula kilichopikwa na mtu mwenye hepatitis C
● Kupiga chafya, kukohoa, kubusiana na kukumbatiana
● Mabwawa ya kuogelea
● Kung’atwa na mnyama au mdudu (kwa mfano mbu)

Tiba, kuongezewa damu na taratibu za
kitabibu na meno viko salama nchini Australia unapofuata kanuni na taratibu zote.

Ninatambuaje kama nina hepatitis C


Watu wengii hawaonekani au kujisikia wagonjwa. Dalili kuu ni kusikia kichefuchefu. Namna pekee ya kutambua ni kupima damu

Ni wakati gani ninaweza kupimwa?


Muulize daktari kuhusu kupimwa kama

● Ulijidunga madawa ya kulevya, hata kama ilikuwa mara ya kwanza ama ilikuwa zamani sana ( Madawa ya kulevya inajumiusha madawa inayotumika kwenye gym)
● Kama ulishakuwa gerezani katika nchi yoyote
● Ulishawekewa ama kuondolewa kiungo ama kuongezewa damu nchini Australia kabla ya mwaka 1990 ama katika nchi nyingine yoyote kabla hawajaanza kupima hepatitis C
● Kama una michoro kwenye mwili ama ngozi iliyotobolewa
● Unatoka nchi yenye idadi kubwa ya watu wenye hepatitis C kama vile Africa, Mashariki ya Kati (hasa Misri), ukanda wa mediterrania, Ulaya mashariki, Asia kusini
● Mama yako ana hepatitis C
● Wewe ni mwanaume, una HIV na una mahusiano ya kingono na wanaume
● Mpenzi wako ana hepatitis C

Je, kirusi cha hepatitis C kinafanya nini ndani ya mwili wangu?


Kirusi cha hepatitis C kinaingia katika seli za ini na kuzalisha virusi zaidi ndani mwake. Mwili unapambana na virusi katika seli za ini kitu ambacho kinaweza kuharibu ini. Wakati mwingine mwili wako wenyewe utapambana na virusi. Hii inaweza kutokea miezi sita tangu ulipopata virusi hivyo

Miili mingi ya watu haiwezi kupambana na virusi vyote. Kwa miaka mingi, lini inaharibika kwa kuwa na makovu mengi. Hii inaitwa ‘Cirrhosis’ na inaweza ikasababisha kansa ya ini na kushindwa kwa ini.

Je, hepatitis C inaweza kutibika?


Ndiyo. Daktari wako anaweza kukupa dawa kutibu hepatitis C

Je, ninalazimika kumwambia mtu yeyote kama nina hepatitis C?


Kwa sheria, ni lazima uwambie wafuatao

● Kama ukitoa damu kwenye benki ya damu
● Kama ukitoa kiungo ama kitu chochote cha majimaji kutoka mwilini mwako kama vile mbegu za kiume.
● Kama kampuni za bima zikikuuliza kama una hepatitis C ama magonjwa mengineyo. Kama usipowambia, hawawezi kukulipa unapofanya madai
● Kama ukitaka kujiunga Jeshi la Ulinzi la Australia (ADF), utalazimika kuwaambia
● Kama wewe ni mfanyakazi wa huduma za afya anayefanya taratibu za kitabibu ambapo huwezi kuiona mikono yako (kama vile upasuaji ama utoaji wa meno), lazima umwambie mwajiri ama msimamizi wako na kupata ushauri kutoka kwa daktari bingwa.

Haulazimiki kumwambia:

● Mkuu wako wa kazi
● Wafanyakazi wenzako ama wanadarasa wenzako
● Familia
● Marafiki

Daktari wako halazimiki kuiambia familia yako

Je, ninawezaje kuepuka kupata hepatitis C?


● Usichangie sindano, sirinji ama vijiko vya chai kujidunga madawa ya kulevya
● Chagua studio za kujichora mwilini na kutoboa mwili kwa umakini sana. Tumia wataalamu wenye leseni. Hakikisha wanatumia sindano na wino mpya kwa kila mteja.
● Tumia kila mara kondomu kama una wapenzi zaidi ya mmoja
● Epuka damu ama matunda ya damu katika nchi ambazo hajichukui vipimo wakati wa kuongeza damu
● Usichangie miswaki na nyembe
● Kama wewe ni mfanyakazi wa afya, kila mara fuata kanuni za tahadhari
Hata kama ulikuwa na hepatitis C siku za nyuma, kila mara fuata kanuni za tahadhari.

Wapi ninaweza kupata msaada na ushauri?


Kuna makundi mengi ya hepatitis C nchini Australia kukupa msaada na ushauri.


Get support from the hepatitis community

More information