STI ni nini?


STI inasimama badala ya vimelea vya maambukizi ya kingono

STIs ni magonjwa unayoyapata unapofanya ngono

Ninapataje STI?


Vimelea vya STI vinaishi katika ngozi, katika damu ama katika majimaji ya via vya uzazi kama vile shahawa, majimaji ya uke.

Unaweza kupata STI kwa kufanya mapenzi(uke, ngono kinyume na maumbile, ngono kwa mdomo) au kugusa via vya uzazi.

Unaweza kupata STI kama usipotumia kondomu.

STI inafanya nini kwa mwili wangu?


Kwa wanawake, STI inaweza kusababisha

● maumivu makali ya tumbo
● Kutokwa uchafu ukeni
● Mabaka karibu na uke
● Mtoto kukua nje ya mji wa mimba
● Mwanamke kujifungua kabla ya wakati (kuporomosha mimba)
● Kichanga kuugua sana

Kwa wanaume, STI inaweza:

● Kumsababishia mwanaume kupata ugumba
● Kutokwa uchafu katika uume
● Kuacha mabaka kwenye uume
● Kusababisha muwasho na maumivu makali unapokojoa (kutoa shahawa)

Ninatambuaje kama nina STI?


Watu wengi hawatambui kama wana STI kwa sababu wanaonekana ama kujisikia vizuri na hawana ishara wala dalili. Namna pekee ya kutambua ni kuchukua vipimo

● mkojo wako unapimwa
● damu yako inapimwa
● Via vyako vinafutwa maambukizi

Unaweza kuhitaji kuchukua kipimo kimoja au vipimo vyote. Daktari wako atakueleza unahitaji kuchukua kipimo kipi.

Je, STI inaweza kutibika na kupona?


Baadhi ya STIs inaweza kupona haraka na kwa urahisi kwa dawa. Baadhi zinaweza kutibiwa lakini siyo kupona.

Unaweza kupata STI tena hata baada ya dawa kuisha na STI kupona

Ni lini ninapawsa kupimwa?


Unapaswa kuchukua vipimo vya STI kama:

● Umefanya mapenzi (kwa uke, kinyume na maumbile ama kwa mazungumzo) bila kutumia kondomu
● Una dalili zozote
● Unafikiri unaweza kuwa na STI
● Kondomu yako ilipasuka ama kuchomoka wakati wa kufanya mapenzi
● Wewe ama mpenzi wako anafanya mapenzi na mtu mwingine
● Wewe ama mpenzi wako alikuwa na wapenzi wengine siku za nyuma
● Unachangia sindano, sirinji, vijiko kujidunga madawa ya kulevya
● Unaanza mahusiano mapya ya kimapenzi

Vipimo vya STI ni nini?


Ni vya haraka, visivyo na maumivu na daima visivyo na gharama. Vipimo hivyo ni tofauti kwa wanaume na wanawake. Daktari ama nesi atachukua kiasi kidogo cha majimaji kwa mfano, mkojo, mate, majimaji ya uke ama damu. Baadhi ya vipimo unaweza kuvifanya mwenyewe.

Inachukua wiki 1 hadi 2 kupata matokeo

Kipimo change kilikuwa “positive.” Ninapaswa kufanya nini?


Kipimo ambacho ni positive kina maana una STI. Daktari atakupatia dawa ambayo ni ya haraka na rahisi kutumia.
Kumbuka, baadhi ya STIs zinaweza kutibiwa lakini siyo kupona kabisa.

Je, ninawajibika kumwambia mtu yeyote nina STI?


Unapaswa kumweleza mpenzi wako na mpenzi wako pia anapaswa kuchukua vipimo. Kama mpenzi wako asipopimwa na asipotumia dawa, mtaendelea kupeana STI

Kama huwezi kumweleza mpenzi wako, mwombe daktari ama nesi awaeleze. Hawatamweleza mpenzi wako kuhusu wewe. Hii inajulikana kama ‘contact tracing.’

Huhitaji kumweleza

● Mkuu wako
● Wafanyakazi wenzako
● Marafiki
● familia

Nifanyeje ili nisimwambukize mwingine STI?


● Usifanye mapenzi mpaka wewe na mpenzi wako mtakapomaliza dawa.
● Tumia kondomu.

Nawezaje kuepuka STI?


Namna sahihi kuepuka kupata STI ni kutumia kondomu kila mara unapofanya mapenzi.

More information