Kaswende ni nini?

Kaswende ni maambukizi ya kingono yanayosababishwa na bakteria ajulikanaye kama Treponema pallidum.

Wanaume na wanawake wanapata kaswende


Ninapataje kaswende?


Unaweza kupata kaswende kwa:
• Kugusa madonda ama ukurutu wa mgonjwa mwenye kaswende hata kama ukurutu huo ni vigumu kuuona
• Kufanya mapenzi kwa kupitia uke, kinyume na maumbile au kwa ngono kwa mdomo
• Kugusana na damu yenye maambukizi
• Mwanamke mjamzito anaweza kukiambukiza kichanga kilicho tumboni.

Kaswende na vichanga (congenital syphilis)


Mwanamke mjamzito anaweza kukiambukiza kichanga kupitia damu. Wakati mwingine, mtoto anaweza kuzaliwa akiwa amekufa ama akiwa na ulemavu.Hii inajulikana kama congenital syphilis na ni nadra sana nchini Australia.

Watoto mara nyingi wanazaliwa wakiwa hawana dalili za syphilis, lakini wanaweza kuugua sana.

Je, ninatambuaje kama nina kaswende?


Mara nyingi hakuna dalili za kaswende, hivyo watu wenye s kaswende wanaweza kujisikia wazima na wenye afya. Ni kwa kupima damu tu unaweza kugundua kama una kaswende.

Wanawake wanapaswa kupima kama wana kaswende katika wiki 12 za mwanzo za ujauzito au wanapomwona daktari wao kwa mara ya kwanza. Baadhi ya wanawake bado wanaweza kupimwa tena baadaye wakati wa ujauzito wao.

Je, ninafanyaje ninapokuwa na kaswende?


• Acha kufanya mapenzi, hata kwa kutumia kondomu, mpaka utakapokamilisha matibabu yako ya kaswende.

• Kama una kaswende, mweleze mpenzi au wapenzi wako ili waweze kupimwa.

Daktari wako atakusaidia kuamua ni nani unalazimika kumwambia kama una kaswende na anaweza kukusaidia kuwaeleza.

Je, kaswende inaweza kutibika au kupona?


• Ndiyo, kaswende inaweza kutibiwa na kupona kwa muda kadhaa wa kuchomwa sindano. Urefu wa matibabu unategemea kaswende yako imefikia hatua gani. Hakikisha unamwona daktari kila mnapokubaliana kukutana.
• Unapokamilisha matibabu yako ya kaswende , unapaswa kupima tena kujiridhisha kwamba umepona.
• Wanawake wanaweza kupata matibabu ya kaswende mapema zaidi katika ujauzito wao kumkinga mtoto na maambukizi ya kaswende .
• Unaweza kupata kaswende tena hata kama ulitibiwa na kupona siku za nyuma.

Je, ninaweza kujilindaje nisiambukizwe kaswende?


• Hakikisha wewe na mpenzi wako mnapima kaswende . Pima mara kwa mara kama una mpenzi Zaidi ya mmoja ama mpenzi ana uhusiano wa kimapenzi na watu wengine. Kadiri ya idadi ya wapenzi unaokuwa nao ndivyo hatari kupata kaswende inavyoongezeka.

• Hakikisha wewe na wapenzi wako mnatibiwa ili msiendee kuambukizana kaswende ama kuwaambukiza watu wengine kaswende .

• Tumia kondomu wakati wa mapenzi kwa njia ya uke, kinyume na maumbile ama kwa ngono kwa mdomo, hata na mpenzi wako wa mda mrefu kama unakuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengine.

• Zungumuza na wapenzi wapya kuhusu kutumia kondomu kabla hujafanya mapenzi nao
• Usifanye mapenzi, hata kwa kondom na mtu mwenye kaswende mpaka matibabu yatakapokamilika.

Je, ninaweza kufanyaje ili nisimwambukize mtu mwingine?


• Usifanye mapenzi na mtu yeyote, hata kwa kutumia kondomu, mpaka matibabu yako yatakapokamilika.
• Pima kaswende mara kwa mara kama una mpenzi zaidi ya mmoja ama mpenzi wako ana mahusiano ya kimapenzi na watu wengine. Unaweza kupata kaswende tena.

Wapi ninaweza kupata msaada na ushauri?


• Daktari
• Kliniki ya afya ya uzazi
• Huduma ya afya ya jamii
• Kituo cha uzazi wa mpango.

More information