Pangusa ni nini?


Pangusa ni maambukizi ya kingono yaliyozoeleka yanayosababishwa na bakteria ijulikanayo kama Chlamydia trachomatis

Ninawezaje kupata pangusa?


Unaweza kupata pangusa kama hautumii kondumu wakati wa kufanya mapenzi kwa njia ya uke, kinyume na maumbile au kwa ngono kwa mdomo na mtu mwenye pangusa.
Huwezi kupata pangusa kutoka vyoo vya umma, mabwawa ya kuogolea ya umma au kuchangamana na watu wengine.

Pangusa inafanya nini kwa mwili wangu?


Kwa wanaume
• Wanaume wanapata pangusa kwenye kibofu (ndani ya uume), utumbo mkubwa au kooni.

• Pangusa inasababisha maumivu na uvimbe kwenye korodani za wanaume na inaweza ikashambulia mfereje wa mbegu.

Kwa wanawake
• Wanawake wanapata pangusa kwenye utumbo mkubwa au kooni. Kama isipotibika, pangusa inaweza kumfanya mwanamke kuwa mgumba.
• Wanawake wenye cpangusa wanaweza wakati mwingine kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua. Hii inaweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye maambukizi ya mapafu na macho.

Ninatambuaje kama nina pangusa?


Watu wengi hawatambui kama wana pangusa kwa sababu hawana ishara au dalili zozote.

Njia rahisi na ya haraka ya kupima mkojo itakueleza kama una pangusa. Unaweza pia kujipima mwenyewe kama una chlamydia

Kwa wanaume

Ishara na dalili za chlamydia kwa wanaume ni zifuatazo:
• Wekundu ama maumivu kwenye mlango wa uume.

• Majeraha au kuwaka moto unapokojoa

• Kutokwa uchafu kwenye uume.

Kwa wanawake

Ishara na dalili kwa wanawake ni zifuatazo:
• Kutokwa uchafu usio wa kawaida kwenye uke

• Kutokwa damu kusiko kwa kawaida

• Uchungu kwa mabavu ya kiuno, haswa wakati wa kufanya mapenzi

• Majeraha au kuwaka moto wakati wa kukojoa.

Ninafanyaje kama nina pangusa?


Pata dawa kutoka kwa daktari
Waeleze wapenzi wako kwamba una pangusa na waombe wachukue vipimo.
Yumkini wapenzi wako pia watakuwa na pangusa na wanaweza kukuambukiza tena.
Wanaweza kuwaambukiza pangusa wengine

Kama mpenzi wako hatachukua vipimo vya pangusa , mwombe daktari dawa za nyongeza kwa ajili yao.

Baada ya miezi mitatu, wewe na mtu mwingine yeyote utakayefanya naye mapenzi apaswa kuchukua vipimo vya pangusa tena.

Je pangusainaweza kutibika ama kupona?


Ndiyo. Ni rahisi sana kuitibu pangusa na kupona kwa kidonge kimoja. Kama c pangusa ikigundulika kwa kuchelewa, itachukua muda kuitibu na kupona
Usifanye mapenzi kwa wiki nzima baada ya kutumia dawa yako ya chlamydia.
Unaweza kupata pangusa tena hata kama ulikwishaipata.

Ninawezaje kujilinda ili nisiambukizwe pangusa?


• Hakikisha wewe na mpenzi wako mnapimwa. Pima mara kwa mara kama una mpenzi zaidi ya mmoja au kama mpenzi wako anafanya mapenzi na watu wengine. Hatari ya kupata pangusa ni kubwa kulingana na idadi ya wapenzi unaokuwa nao.
• Pata matibabu: Mwombe mpenzi wako kupima na kutibiwa pia ili msiendelea kuambukizana au kuwaambukiza watu wengine.

• Tumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi kwa uke, kinyume na maumbile au kwa ngono kwa mdomo.
• Zungumza na wapenzi wako kuhusu kutumia kondomu kabla ya kufanya mapenzi.

Ninawezaje kuhakikisha simwambukizi mtu mwingine pangusa?


• Tumia kondomu kila mara unapofanya mapenzi, hasa unapofanya mapenzi na mpenzi mpya.
• Pima kila mara kama una mpenzi zaidi ya mmoja au mpenzi wako anafanya mapenzi na watu wengine. Unaweza kupata pangusa tena hata kama ulishakuwa nayo.

Wapi ninaweza kupata msaada na ushauri?


• Daktari
• Kliniki ya afya ya uzazi
• Huduma ya afya ya jamii
• Kituo cha uzazi wa mpango.

More information